logo

Tag : habari

19 Jan 2018

Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, amenyimwa dhamana tena na amerudishwa rumande hadi 22 Jan 2018.

Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi “Sugu’’ pamoja na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga, wamerudishwa rumande hadi Jumatatu ijayo ambapo kesi yao ya kutoa matamshi ya uchochezi itaanza kusikilizwa mfululizo. Wawili hao, walifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza Jumanne tarehe 16 Januari, 2018 katika Mahakama ya Mkoa wa Mbeya na mahakama iliwanyima dhamana na kuamuru wapelekwe rumande mpaka tarehe 19 Januari 2018(leo) ambapo pia wamenyimwa dhamana hadi Jumatatu.  

11 Jan 2018
11 Jan 2018

Mamlaka ya Hali ya Hewa:Mvua kubwa kunyesha tena ndani ya siku Tatu

Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) imetahadharisha kunyesha kwa mvua kubwa kuanzia usiku wa  tarehe 10/01/2018 hadi  tarehe 13/01/2018 Mvua hizo zitaathiri Ukanda wa Pwani na Kusini zikianzia mikoa ya Lindi na Mtwara na kusambaa maeneo ya Morogoro kusini.

18 Dec 2017

Watu 18 wauawa kufuatia vita kati ya waasi na majeshi ya Sudan Kusini

Watu kumi na wanane wameuawa kufuatia mapigano kati ya vikosi vya usalama vya Sudan Kusini na waasi watiifu kwa makamu wa rais wa zamani Riek Machar. Maafisa wa serikali wamesema hayo leo na kuongeza mapigano yalitokea Jumamosi usiku katika eneo la Upper Nile. Msemaji wa jeshi Santo Domic Chol ameliambia shirika la habari la ujerumani DPA kwamba wanajeshi wanane wameuawa pamoja na waasi 10, kufuatia shambulio ambalo lilifanywa katika kambi ya jeshi ililoko jimbo la Latjor. Msemaji wa waasi Paul […]

18 Dec 2017

Russia yaitahadharisha Marekani

Victor Bondarev Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Baraza la Shirikisho la Russia ameeleza kuwa Marekani inafanya kila iwezalo ili kuvuruga tena hali ya mambo huko Syria na kwamba Russia itamsaidia Rais Bashar al Assad wa nchi hiyo kupambana na suala hilo. Seneta Viktor Bondarev amesisitiza kuwa serikali ya Syria ina nguvu za kutosha za kukabiliana na njama za Marekani na haitatoa mwanya wa kuitumbukiza tena Syria katika hali ya mchafukoge. Wizara ya Ulinzi ya Russia pia jana […]

18 Dec 2017

Mkutano mkuu wa CCM kufanyika leo mjini Dodoma

Mkutano mkuu wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi  unaanza leo mjini Dodoma ukiwa na lengo la kumchagua Mwenyekiti wa Chama na Makamu wake wawili kutoka Tanzania bara na Zanzibar.

18 Dec 2017
17 Dec 2017

Wito watolewa kuharakisha kuuawa wabakaji Nchini India

 Mteteaji mkuu wa haki za wanawake India amependekeza kuwa wabakaji wa watoto wanapaswa kuuawa katika muda wa miezi sita tangu watekeleza uovu huo. Swati Maliwal ametoa ombi hilo katika barua aliyomuandikia waziri mkuu Narendra Modi. Iliandikwa kuendana na kumbukumbu ya mwaka wa tano tangu mwanafunzi Jyoti Singh mwenye umri wa miaka 23 alipobakwa na gengi la wanaume, kifo chake kilichozusha maandamano ya kitaifa. “Hakuna kilichobadilika kaika miaka mitano iliyopita,” Bi Maliwal, alisema. “Delhi bado ndio mji mkuu wa ubakaji. Mwezi […]

24 Nov 2017

Dr Slaa ateuliwa kuwa balozi

Aliyekuwa Katibu mkuu wa chama cha upinzani CHADEMA ameteuliwa kuwa balozi na Rais wa Tanzania, John Magufuli. Katika taarifa ilitolewa na Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu ,Gerson Msigwa, haijataja kituo chake cha kazi. Ila imeeleza “ataapishwa baada ya taratibu kukamilika” Dokta Wilbord Slaa alikuwa kiongozi muandamizi wa upinzani nchini Tanzania. Alijiuzulu nafasi ya ukatibu mkuu na uanachama wa Chadema mwaka 2015 baada ya ujio wa waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye alipewa nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho […]

24 Nov 2017

Kiongozi mpya wa Zimbabwe kuapishwa

Emmerson Mnangagwa anatarajiwa kuapishwa kama rais wa Zimbabwe, kufuatia kuondoka kwa rais Robert Mugabe madarakani baada ya miaka 37 ya utawala wa kiimla. Makamu huyo wa zamani wa rais ambaye alirejea kutoka uhamishoni Jumatano -ataapishwa katika uwanja wa ndege wa Harare. Kufutwa kwake kazi mwezi huu kulipelekea chama tawala cha Zanu-PF na jeshi kuingilia kati na kumlazimisha Mugabe ang’atuke . Upinzani unamtaka Bwana Mnangagwa, ambae amekuwa mmoja wa watawala kumaliza “utamaduni wa ufisadi”. Taarifa ya kuondoka madarakani kwa Mugabe mwenye […]