logo

Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, amenyimwa dhamana tena na amerudishwa rumande hadi 22 Jan 2018.

Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi “Sugu’’ pamoja na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga, wamerudishwa rumande hadi Jumatatu ijayo ambapo kesi yao ya kutoa matamshi ya uchochezi itaanza kusikilizwa mfululizo.

Wawili hao, walifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza Jumanne tarehe 16 Januari, 2018 katika Mahakama ya Mkoa wa Mbeya na mahakama iliwanyima dhamana na kuamuru wapelekwe rumande mpaka tarehe 19 Januari 2018(leo) ambapo pia wamenyimwa dhamana hadi Jumatatu.

 

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *