logo

Russia yaitahadharisha Marekani

Victor Bondarev Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Baraza la Shirikisho la Russia ameeleza kuwa Marekani inafanya kila iwezalo ili kuvuruga tena hali ya mambo huko Syria na kwamba Russia itamsaidia Rais Bashar al Assad wa nchi hiyo kupambana na suala hilo.

Seneta Viktor Bondarev amesisitiza kuwa serikali ya Syria ina nguvu za kutosha za kukabiliana na njama za Marekani na haitatoa mwanya wa kuitumbukiza tena Syria katika hali ya mchafukoge. Wizara ya Ulinzi ya Russia pia jana ilitangaza kuwa Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) inashiriki katika kuwapatia mafunzo na kuwapa msaada magaidi huko Syria.

 

Taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Russia imeongeza kuwa Pentagon tangu miezi sita iliyopita ilianza kuyapatia misaada ya hali na mali makundi ya kigaidi katika kambi za mafunzo zilizopo katika mkoa wa al Hasakah huko Syria. Wizara ya Ulinzi ya Russia aidha imeripoti kuwa karibu magaidi 800 wamepata mafunzo kwenye kambi hizo na kwamba magaidi hao wanatazamiwa kuhamishiwa katika maeneo ya kusini mwa Syria.

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *