logo

Wito watolewa kuharakisha kuuawa wabakaji Nchini India

 Mteteaji mkuu wa haki za wanawake India amependekeza kuwa wabakaji wa watoto wanapaswa kuuawa katika muda wa miezi sita tangu watekeleza uovu huo.

Swati Maliwal ametoa ombi hilo katika barua aliyomuandikia waziri mkuu Narendra Modi.

Iliandikwa kuendana na kumbukumbu ya mwaka wa tano tangu mwanafunzi Jyoti Singh mwenye umri wa miaka 23 alipobakwa na gengi la wanaume, kifo chake kilichozusha maandamano ya kitaifa.

“Hakuna kilichobadilika kaika miaka mitano iliyopita,” Bi Maliwal, alisema.

“Delhi bado ndio mji mkuu wa ubakaji. Mwezi uliopita, mtoto wa kike wa mwaka mmoja na nusu alibakwa na gengi la wanaume, na ubakaji wa mtoto wa miaka saba,na mwingine wa kike wa mwaka mmoja na nusu alibakwa.”

Kwa wastani, alisema, watoto watatu wa kike na wanawake wasita wanabakwa katika mji mkuu huo kila siku.

India ilifanyia mageuzi sheria zake kuhusu ubakaji kutokana na shutuma miaka mitano iliopita, na ilichukua hatua kuharakisha kusikilizwa kesi na kuwashinikiza maafisa wa polisi kutilia uzito tuhuma za ubakaji na unyanyasaji wa kingono.

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *