logo

Kiongozi mpya wa Zimbabwe kuapishwa

Emmerson Mnangagwa anatarajiwa kuapishwa kama rais wa Zimbabwe, kufuatia kuondoka kwa rais Robert Mugabe madarakani baada ya miaka 37 ya utawala wa kiimla.

Makamu huyo wa zamani wa rais ambaye alirejea kutoka uhamishoni Jumatano -ataapishwa katika uwanja wa ndege wa Harare.

Kufutwa kwake kazi mwezi huu kulipelekea chama tawala cha Zanu-PF na jeshi kuingilia kati na kumlazimisha Mugabe ang’atuke .

Upinzani unamtaka Bwana Mnangagwa, ambae amekuwa mmoja wa watawala kumaliza “utamaduni wa ufisadi”.

Taarifa ya kuondoka madarakani kwa Mugabe mwenye umri wa miaka 93 hapo siku ya Jumanne kuliibua sherehe kubwa kote nchini Zimbabwe

Ilitolewa kwa njia ya barua bungeni na kikao cha kumpigia kura ya kutokuwa na imani nae kikakatizwa.

Katika barua hiyo Bwana Mugabe alisema anajiuzulu ili kuruhusu mchakato rahisi na wa amani wa ukabidhianaji mamlaka na kwamba uamuzi wake ulikuwa wa hiari.

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *