logo

Watu 50 wauawa katika mripuko wa bomu msikitini nchini Nigeria

Takribani watu 50 wameuawa katika shambulio la bomu dhidi ya msikiti mmoja ulioko kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Msemaji wa Polisi katika jimbo la Adamawa, Othman Abubakar amesema mripuko huo umetokea  katika mji wa Mubi, wakati Waumini wa Kiislamu walipokuwa wakiingia msikitini hapo kwa ajili ya Sala ya alfajiri.

Amesema kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram ndilo limehusika na shambulizi hilo, na kwamba idadi ya watu waliojeruhiwa ni kubwa mno ingawaje hawana takwimu rasmi kwa sasa.

Naye Bayi Muhammad, mmoja wa waumini wanaokwenda katika msikiti huo na ambaye ameshuhudia tukio hilo amesema baadhi ya wahanga wa hujuma hiyo ya kikatili wameteketea kiasi cha kutotambulika.

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *