logo

UEFA:Madrid,Tottenham na Man City zaendeleza ubabe

Michuano ya Kombe la vilabu bingwa barani ulaya iliendelea jana huku ikishuhudiwa baadhi ya Timu zikiendeleza  rekodi nzuri ya ushindi tangu kuanza kwa michuano hiyo msimu huu.Mabingwa watetezi Real Madrid kutoka Hispania jana wakiwa ugenini walipata ushindi wa mabao sita dhidi ya APOEL Nicosia,Magoli ya Karim Benzema,Ronaldo na Modric yaliiwezesha miamba hiyo ya Hispania kuibuka na ushindi mnono siku ya jana.

Katika michuano ya msimu huu kumeshuhudiwa mabadiliko kutoka kwa timu za Uingereza ambazo zimendeelea kufanya vizuri jana Manchester City walipata ushindi wa bao moja dhidi ya Feyenood lililofungwa na Raheem Sterling.

Nao Tottenham Hotspurs wakiwa ugenini dhidi ya Borussia Dortmund waliibuka na ushindi wa maba0 mawili kwa moja.Delle ali alikuwa mwiba mchungu kwa Borussia huku akitengeneza nafasi zilizozaa mabao yote mawili ya spurs.

 

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *