logo

Mahakama yaidhinisha ushindi wa Kenyatta Kenya

Uamuzi wa mahakama ya juu wa kuidhinishwa kwa ushindi wa rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa Oktoba 26 umezua maandamano ya ghasia katika maeneo yanayodaiwa kuwa ngome za upinzani nchini Kenuya.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation wafuasi wa kiongozi wa muungano wa Nasa Raila Odinga waliandamana ili kuonyesha kutoridhishwa kwao na uamuzi huo.

Maandamano hayo yalibadilika na kuwa ya ghasia katika maeneo kadhaa ya Nyanza, nyumbani kwa Odinga , katika maeneo ya Kibira na Mathare mjini Nairobi.

Mjini Kisumu, gari moja la kibinafsi lilichomwa katika eneo la Kondele muda mfupi baada ya ghasia kuzuka katika mji huo wa ziwa Victoria kufuatia uamuzi huo wa mahakama.

kulingana na gazeti hilo vijana walifunga barabara zinazoelekea mjini Kisumu kwa kuchoma magurudumu ya gari na mawe.

Waliwazuia watu watatu waliokuwa katika gari hilo la kibinafsi , wakawapiga na kuwaibia kabla ya kuliharibu gari hilo na kulichoma.

Watatu hao walikimbilia katika kituo cha polisi cha kondele wakihofia maisha yao.

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *