logo

Amuua mkewe kwa kukataa kushiriki tendo la ndoa

Maafisa wa polisi wanasema kuwa mwanamume mmoja katika jimbo la kaskazini mwa India la Haryana amemuua mkewe baada ya kukataa kushiriki naye tendo la ndoa.

Sanjiv Kumar mwenye umri wa miaka 35 alidaiwa kumyonga mkewe ,Suman wakati wa vita siku ya Jumanne.

Mwanamume huyo alikiri kutekeleza kitendo hicho baada ya kukamatwa , afisa wa polisi Ramesh Jaglan aliiambia BBC.

Migogoro ya kiyumbani ndio yenye visa vingi vilivyoripotiwa dhidi ya wanawake nchini India kwa zaidi ya muongo mmoja sasa.

”Alikuwa akikataa kufanya ngono kwa muda .Siku ya Jumanne alikataa tena, hatua iliomuudhi na kuamua kumnyonga.Tumemkamata”, bwana Jaglan alisema.

Wanandoa hao walikuwa wameoana kwa zaidi ya muongo mmoja. Wana watoto wawili.

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *