logo

Kinachoendelea Zimbabwe:Waandamanaji wapiga kambi nje ya makao ya Mugabe

Waandamanaji nchini Zimbabwe wameelekea katika ofisi ya rais Mugabe ili kumtaka kujiuzulu.

Maandamano hayo yanajiri kufuatia furaha ilioonekana miongoni mwa raia baada ya jeshi kuingilia kati na kumzuia rais Mugabe kwa muda nyumbani kwake siku ya Jumatano.

Wanajeshi katika ikulu ya Whitehouse walioonekana wakiwarudisha nyuma waandamanaji.

Jeshi liliingilia kati baada ya rais Mugabe kumfuta kazi makamu wake wa urais , akionyesha ishara za kutaka mkewe kumrithi.

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *