logo

Tetemeko nchini Iran na Iraq laua zaidi ya watu 100

Tetemeko la ukubwa wa 7.3 katika vipimo vya richa limekumba eneo la kaskazini mwa Iran na Iraq na kuua watu kadhaa.

Takriban watu 129 waliuawa katika mkoa ulio magharibi mwa Iran wa Kermanshah, kwa mujibu wa maafisa.

Tetemeko hilo lilizua hofu hadi kusababisha watu kukimbia kutoka majumbani mwao na kwenda barabarani.

Misikiti kwenye mji mkuu wa Iraq Baghdad, imekuwa ikifanya maombi kwa kutumia vipasa sauti.

 

Wengi wa waathiriwa walikuwa ni kwenye mji wa Sarpol-e Zahab, kilomita 15 kutoka mpakani.

Kulingana na kituo cha Marekani USGS tetekemo hilo lilitokea umbali wa kilomita 33.9 chini ya ardhi la lilisikika nchini Uturuki, Israel na Kuwait.

Uharibifu umeripotiwa kutokea katika vijiji vinane kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu nchini Iran .

Baadhi ya vijiji vimekumbwa na matatizo ya nguvu za umeme na mawasiliano yamevurugwa.

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *