logo

Mlipuko Kagera waua wanafunzi sita

Wanafunzi sita wa shule ya msingi Kihinga mkoani Kagera kaskazini magharibi mwa Tanzania wamefariki dunia na wengine 41 wamejeruhiwa baada ya kulipukiwa na bomu wakicheza.

Kamanda wa polisi wa mkoa, Augustine Oromi huo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari wananchi wamejitokeza kuchangia damu kwa ajili ya kuwasaidia majeruhi.

Mkoa wa Kagera ni eneo linalowahifadhi wakimbizi kutoka nchi jirani kama Burundi. Baadhi ya wakimbizi hao walikuwa wanajeshi ambao waliacha silaha zao katika baadhi ya makambi.

Kamanda wa polisi wa mkoa, Augustine Oromi amesema tayari timu ya upelelezi imetumwa katika eneo hilo kuchunguza sehemu ambapo bomu lililipukia.

Kwa mujibu wa Dokta Mariagoreth Fredrick ambaye ni mganga mkuu hosipitali ya Rulenge, amethibitisha kupokea miili hiyo na majeruhi ambao baadhi wako katika hali mbaya na tayari wanapatiwa matibabu.

“Tulionao hali ya sio nzuri. Wengine wameumia matumbo, wengine wamechanika bandama, wengine wamevunjika miguu, wengine vichwa vimepata majeraha, wengine wameumia macho.” Dokta Mariagoreth alieleza.

Inaelezwa kwamba kabla ya kulipukiwa na kifaa hicho kinachoarifiwa kuwa ni bomu, wanafunzi hao walikuwa wanakichezea.

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *