logo

Mwanamke afukuzwa kazi kwa kuuonyesha msafara wa Rais Trump kidole cha kati

Mwanamke aliyepigwa picha akiuonyesha msafara wa rais Donald Trump ishara ya kidole cha kati ameripotiwa kufutwa kazi na kampuni iliomuajiri kufutia picha hiyo.

Picha hiyo ilisambazwa baada ya kupigwa mnamo terehe 28 mwezi Oktoba mjini Virginia karibu na uwanja wa kucheza Gofu wa Trump.

Juli Briskman ambaye alitambulika kama mwendesha baiskeli anadai kwamba alifutwa kazi na mwajiri wake Akima LLC baada ya kuichapisha katika mtandao wake.

Kampuni hiyo hata hivyo haikutoa tamko lolote.

Bi Briskman aliviambia vyombo vya habari kwamba kampuni hiyo ilimuita katika mkutano siku moja baada ya kumwambia afisa mkuu wa ajira kwamba ni yeye ndiye aliyepiga picha hiyo.

Alilimbia gazeti la Huffington Post kwamba maafisa wakuu wa kampuni hiyo walimwambia kwamba picha hiyo imeorodheshwa kama chafu na kwamba ilikiuka viwango vya sera za mitandao baada ya kuichapisha katika akaunti zake za Twitter na facebook.

Hatahivyo bi Briskman alisema kuwa aliusisitizia usimamizi wa kampuni hiyo kwamba hakuwa akifanya kazi wakati picha hiyo ilipopigwa na kwamba hakuwataja waajiri wake katika mtandao huo wa kijamii.

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *