logo

Watu 26 wauawa kwa kupigwa risasi kanisani Texas, Marekani

Watu 26 wameuawa kwa kupigwa risasi na mtu mwenye silaha aliyewafyatulia risasi waumini katika kanisa moja jimbo la Texas wakati wa ibada, maafisa wanasema.

Shambulio hilo lilitekelezwa katika kanisa la First Baptist Church katika mji wa Sutherland Springs, mji mdogo katika wilaya ya Wilson, Texas.

Mshambuliaji, ambaye anadaiwa kuuawa baada ya kutekeleza mauaji hayo, aliingia kanisani na kuanza kuwafyatulia risasi watu mwendo wa saa tano unusu asubuhi .

Gavana Greg Abbott amethibitisha idadi ya waliofariki na kusema ndicho kisa kibaya zaidi cha mauaji ya kutekelezwa kwa kutumia bunduki katika historia ya texas.

“Kutakuwa na majonzi na masikitiko mengi kwa wale walioathiriwa,” aliwaambia wanahabari.

Mkuu wa idara ya usalama wa Texas Freeman Martin amesema waathiriwa walikuwa na umri wa kati ya miaka 5 na 72.

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *