logo

Angola yawatimua maelfu ya wahamiaji haramu wa Congo DR

Serikali ya Angola imewafukuza nchini humo maelfu ya wahamiaji haramu raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Shirika rasmi la habari la Angola ANGOP limeripoti habari hizo na kuongeza kuwa, wahajiri hao haramu wapatao 2,884 walikamatwa katika mkoa wa Lunda Norte, mpakani mwa nchi hizo mbili , kati ya mwezi Septemba na Oktoba mwaka huu.

Mkuu wa Polisi katika mkoa huo, Rodrigues Zeca ameliambia shirika hilo la habari kuwa, katika operesheni hiyo ya maafisa usalama mkoani hapo,  Wakongomani wengine 10,128 waliamua kurejea nchini kwao kwa hiari.

Amesema aghalabu ya wahamiaji hao haramu huingia nchini Angola kwa ajili ya kutafuta madini hususan ya almasi katika mikoa ya Lunda Norte na Lunda.

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *