logo

UEFA: Man U yaichapa Benfica,Barcelona yalazimishwa sare ya bila kufungana na Olympiacos.

Manchester United ikiwa nyumbani katika dimba la Old Trafford imefanikiwa kuichapa Benfica 2-0 na kwa mara ya kwanza ndani ya miaka minne inaweza kuingia katika hatua ya mtoano.
United ambayo imeingia katika mashindano hayo kwa kuchukua kikombe cha ligi ya Europa msimu uliopita wameshinda michezo yote minne waliocheza na hivyo wanahitaji alama moja pekee katika michezo miwili iliyosalia ili kuweza kufuzu moja kwa moja.
Anthony Martial, ambaye alikuwa tishio katika mchezo huo, alikosa mkwaju wa penalti baada ya kuangushwa katika eneo la hatari na Douglas na mkwaju wake kuchezwa na mlinda mlango wa Benfica Mile Svilar ambaye alikuwa katika kiwango kizuri.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *