logo

Tunataka uchaguzi urudiwe – Raila Odinga

Kiongozi wa Vyama vya Upinzani nchini Kenya, Raila Odinga ameitaka Tume ya Uchaguzi nchini humo (IEBC) kuitisha uchaguzi mwingine wa huru na wa haki ndani ya siku 90 kuanzia jana.

Raila Odinga

Odinga ameyasema hayo jana kwenye mkutano na wafuasi wake jijini Nairobi, ambapo amedai uchaguzi uliofanyika tarehe 26 Oktoba haukuwa wa haki na kuiamuru IEBC kutangaza upya uchaguzi mwingine.

Sisi (Wapinzani) tunataka uchaguzi urudiwe ndani ya siku 90 kwani ndio utakuwa uchaguzi wa haki na huru. Mnasema Wakenya wamechoshwa na uchaguzi lakini nimewambia nao wamesema wamechoshwa na uchaguzi uliogubikwa na hujuma wanataka uchaguzi uliokuwa wa haki.“amesema Odinga kwenye mkutano na wafuasi wake katika eneo la  Kawangware, jijini Nairobi.

Kwa upande mwingine, mgombea mwenza wa Rais Uhuru Kenyatta, Ndg William Ruto amesema kwa sasa Kenya haiwezi kufanya tena uchaguzi hadi mwaka 2022.

 

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *