logo

Mh. Zitto ashusha neema kwa wanafunzi wa Kigoma Ujiji

Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe amewatakia kheri ya wanafunzi wanaofanya mitihani ya kidato cha nne Tanzania nzima kuanzia Leo huku akiwaambia wanafunzi wanaotoka Manispaa ya Kigoma Ujiji, wanachotakiwa ni kufaulu tu, kidato cha tano na sita watasoma bure.

Mhe. Zitto amesema kuwa wanafunzi hao wa Kigoma Ujiji watasoma bure huku manispaa zao zikiwalipia.

Kwa wanafunzi wanaofanya mitihani ya kidato cha Nne Tanzania nzima kuanzia Leo nawatakia kila la kheri. Mola awafanyie wepesi mfanye vizuri mitihani yenu.
Kwa wale wanaotoka Manispaa ya Kigoma Ujiji, mnajua mnachotakiwa ni kufaulu tu. Kidato cha Tano na cha Sita utasoma bure, manispaa yako inakulipia. Hii ndio tofauti yenu na wenzenu kutoka sehemu nyengine ya nchi yetu.
Ninyi mnaofanya mitihani Leo kutokea Kigoma, pia mtakapomaliza kidato cha sita mtakuta utekelezaji wa ufadhili wa elimu ya juu. Tunataka msimalize masomo yenu na mikopo. Utekelezaji wa Miradi yetu utakapo kamilika, mtapewa scholarship kwenda vyuo vikuu na manispaa yenu na kuondokana na adha za mikopo ambazo kaka na dada zenu wanapata Hivi sasa.
Mitihani mema kwenu nyote

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *