logo

Catalonia yaidhalilisha Madrid

Mabingwa wa klabu bingwa barani Ulaya na mabingwa watetezi wa La Liga klabu ya Real Madrid hapo jana usiku imekubali kipigo cha aibu kutoka kwa timu dhaifu ya Girona inayopatikana Jimbo la Catalonia inayoshiriki ligi ya Hispania.

Madrid imeonekana ikihaha kuchomoa bao la pili lililofungwa na timu ya Girona katika mchezo huo uliyomalizika kwa mabao 2-1.

Waliyo kuwa mashujaa katika mchezo huo kwa upande wa Girona alikuwa ni aliyekuwa straika wa Middlesbrough, Cristhian Stuani akifunga bao la kwanza dakika ya 54 kisha, Portugues Manzanera akitupia la pili dakika ya 58 waka la Madrid likifungwa na Isco dakika ya 12 ya mchezo.

Vijana wa Catalonia kikosi cha Gironanidhaifu zaidi ukilinganisha na kile cha Real Madrid, ikiwa imeanzishwa mwaka 1930 kimesheheni wachezaji wa mkopo na waliyosajiliwa wakiwa huru kutoka katika timu zao.

Girona haina taji kuwa hata moja ukilinganisha na Madrid yenye mataji 85, kikosi chake kikiwa na gharama ya paundi milioni 37 huku Real ikiwa ni paundi milio 657 huku Uwanja wao wa nyumbani ukibeba watu 13,500 tofauti kabisa na Santiago Bernabeu ukiwa una uwezo wa kuchukuwa watu 81,000.

Kwa matokeo hayo inakifanya kikosi cha Zinedine Zidane kushuka hadi nafasi ya tatu ikiwa na pointi 20 chini ya Barca wemye pointi 28 na Valencia pointi 24 ambazo hazijapoteza katika michezo 10 iliyocheza mpaka sasa.

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *